Sibuka FM

watu watatu wajeruhiwa na chui

19 October 2021, 3:38 pm

Kwenye picha ni RPC mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda

Watu watatu wakazi wa Kijiji Mwabulimbu kata ya Mwan’gonoli tarafa ya Sengerema wilayani Maswa mkoani Simiyu wamejeruhiwa na mnyama aina ya chui sehemu mbalimbali za miili yao.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 18/10/2021 majira ya saa 8:00 asubuhi wakati mmoja wahanga wa tukio hilo akiwa anachunga ng’ombe majarubani ambapo waliojeruhiwa na chui huyo ni Mashindike Gambalala umri wa miaka 45 mkulima, Kurwa Milima umri miaka 28 mkulima, na Japhet Milima umri  wa miaka 13 ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi Mwabulimbu,  wote wakiwa ni wasukuma na wakazi wa Mwabulimbu.

Kamanda Chatanda ameongeza kuwa mmoja wa majeruhi hao Japhet Milima alimuona chui huyo akiwa anachunga ng’ombe na kupiga kelele za kuomba msaada baada ya chui huyo kuanza kumshambulia na ndipo kundi la watu lilifika na kuanza kumshambulia chui huyo kwa kutumia silaha za jadi ikiwa ni mapanga, fimbo, mawe, na mikuki na walifanikiwa kumuua chui huyo.

Sauti ya RPC mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda akitoa taarifa ya kujeruhiwa na chui watu watatu

Majeruhi wote walipelekwa kituo cha afya Malampaka kwa ajili ya matibabu na hali zao zikiripotiwa kuendelea vizuri.

Aidha maafisa wa maaliasili na wahifadhi misitu wa halmashauri ya wilaya ya Maswa walimchukua chui huyo baada ya kuuwawa kwa kushambuliwa na wananchi.