Sibuka FM

mkoa wa simiyu na mkakati wa kuzalisha tani laki tano za pamba msimu wa kilimo 2021/2021

12 October 2021, 9:44 am

Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila amewaomba wadau mbalimbali wa zao la pamba mkoa hapo  kuhakikisha  mkakati wa  zao hilo wa  kuzalisha tani laki tano za pamba unatekelezwa kwa vitendo na siyo kwa makaratasi lengo nikuongeza thamani ya zao hilo Pamoja na  kuiwezesha  Tanzania  kuwa  kinara  wa zao la pamba barani Afrika na hatimaye kuingia kumi bora duniani.  

kwenye picha ni mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akiwa kwenye kikao kazi na wadau mbalimbali wa kilimo cha zao la pamba wilayani Meatu


David Kafulila ameyasema hayo wakati wa kikao  cha  wadau mbalimbali wa kilimo cha pamba  cha tathimini kilichofanyika  wilayani Meatu na kuongeza kuwa ili kufikia malengo ya mkoa ya kuzalisha tani laki tano lazima kila mdau wa pamba kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila

Juma Topera  ni katibu tawala msaidizi uchumi na uwezeshaji mkoa wa Simiyu amesema kuwa katika kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa kinara wa uzalishaji wa pamba barani afrika kuna sababu ya mkoa huo kufanya kilimo chenye tija.

sauti ya katibu tawala msaidiziuchumi na uwezeshaji mkoa wa Simiyu,Juma Topera

Naye mkuu wa wilaya hiyo Fauzia Hamidu amezitaja changamoto walizokutana nazo kipindi  cha kutoa  elimu ya uhamasishaji kuwa ni pamoja na baadhi ya jamii kudai uhaba wa samadi kutokana na kutokuwa na ng’ombe wa kutosha sambamba na uwepo wa tembo  katika maeneo yao hatua inayopelekea kukatishwa tamaa.

sauti ya Fauzia Hamidu ambaye ni mkuu wa wilaya ya Meatu

Kwa upande wake afisa kilimo kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa huo Kija Kayenze  ametaja baadhi ya mikakati  kuwa ni pamoja na kufanya uhamasishaji kupitia mikutano ya hadhara,kupokea maelekezo kutoka ngazi ya mkoa hadi ngazi ya kijiji , kujadili na kufanya tathimini kila baada ya wiki mbili .
Mkoa wa Simiyu unazalisha nusu ya pamba yote nchini huku wilaya ya Meatu ikitajwa kuongoza kwa uzalishaji kwa wilaya zote nchini.