Sibuka FM

NMB yatoa Msaada wa vifaa vya ujenzi Shule za Msingi na Sekondari Maswa.

8 October 2021, 7:15 pm

Benki  ya  NMB   imekabidhi  vifaa  vya  Ujenzi  kwa  Shule  za  Msingi  na  Sekondari  Wilayani  Maswa   Mkoani  Simiyu  vyenye  thamani  ya  Shilingi  Milioni  Ishirini  na  Nne..

Akikabidhi  vifaa  hivyo mbele  ya  Mkuu  wa Wilaya  ya  Maswa Mh   Aswege  Kaminyoge ,  Meneja   wa  Benki  ya  NMB  kanda  ya  Magharibi  Ndugu   Sospeter  Magesse  amesema  kuwa   vifaa  hivyo  vitasaidia  kukamilisha  Ujenzi  wa    vyumba  vya  Madarasa  na  kupunguza   adha  ya  Michango  kwa  Wananchi..

Sauti ya Meneja NMB kanda ya Magharibi- Sospeter Magesse

                  

Bwana  Magesse  amezitaja  shule  zilizopata misaada  hiyo  na  kusema  kuwa   Benki  ya  NMB  imekuwa  na  utaratibu  wa  kila mwaka   kurudisha  asilimia    ya  faida  yake  kwa  Wananchi na  kuzielekeza  katika   sekta  ya  Elimu  na  Afya.

Sauti ya Meneja NMB kanda ya Magharibi- Sospeter Magesse

                

Akipokea  vifaa hivyo  kwa  Niaba  ya  wananchi  Mkuu  wa  wilaya  ya  Maswa Mh  Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa  anawashukuru  Benki  ya  NMB  na  kuahidi   kuvitunza  na  kutumika  kama  ilivyoelekezwa  huku  akimwelekeza  Mkurugenzi  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa   kutatua  changamoto  za  miundo  mbinu  ya  Barabara , Umeme  na  maji katika  shule  hiyo  ya Msingi  Mwawai ..

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge

                 

Kwa upande  wake   Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  Mh  Paul Maige   amesema  kuwa  NMB  imeonyesha  mfano  kwa  kuunga  mkono  jitihada za  Serikali   za  ujenzi  wa  vyumba  vya  madarasa  na  kuleta  maendeleo  kwa  wananchi..

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri Maswa Paul Maige

              

Wakitoa  shukurani  zao  kwa  Benki   baadhi  ya  wanafunzi  wa  shule  ya  Mshingi  Mwawai  wamesema kuwa  vifaa  hivyo  vitawasaidia  kukaa  kwenye  madarasa  bila  kubanana  na  kuwafanya  wasome  vizuri  huku  wakielekeza  kilio  chao  kwa  serikali  kuwaboresha  miundombinu  ya  Barabara  kwani  kipindi  cha  Masika  kumekuwa  hakufikiki  shuleni  hapo…

Sauti za Baadhi ya wanafunzi wa Mwawai

         

Hapa chini ni picha za matukio ya kukabidhi vifaa vya Ujenzi- shule ya Msingi Mwawai