Sibuka FM

RC Kafulila; Bei ya Pamba yavunja rekodi Msimu wa 2020/2021.

September 17, 2021, 4:56 pm

Mkuu wa  mkoa  wa  Simiyu  Mh,  Davidi  Zacharia  Kafulila  amesema  kuwa  bei  ya  Pamba  kwa  mwaka  huu  wa  2021  imevunja   rekodi  ya   zaidi  ya  miaka Ishirini  iliyopita  kutokana  na  Usimamizi  Bora wa mifumo  ya  ununuzi  wa   zao  la  Pamba..

Mh  Kafulila  amesema   kuwa  kupanda  kwa  bei  ya  Pamba  imetokana  na  maelekezo  ya   Rais  wa  awamu  ya  sita  Mh  Samia  Suruhu  Hasani kwamba  hakuna ujanja  ujanja  katika  bei kwakuwa  wakulima  wengi  hawajui  bei  ya  Pamba  katika soko  la  Dunia.

Sauti ya RC Kafulila

Aidha  mkoa wa  Simiyu  umepokea   nyingi  kwa  ajili  ya  shughuli  za  maendeleo  ambapo amewataka  viongozi  wenzake  kusimamia  fedha  hizo   ili zilete tija  kwa  wananchi .

Sauti ya RC Kafulila

Mh  Kafulila  akiwa  katika  ziara  yake  wilayani  Meatu   amefanya  mikutano  ya  hadhara  katika maeneo  mbali mbali  na  kusikiliza  kero  za  wananchi ikiwa  ni  utaratibu  aliojiwekea  huku  hoja  zikiibuka  katika sekta  ya  Pamba, Afya na  Elimu.

Wananchi wilayani Meatu
RC Kafulila
Wananchi -Meatu