Sibuka FM

TARURA Maswa Kuboresha Barabara zote za Kiuchumi

28 August 2021, 8:36 pm

Meneja  wa  Wakala  wa  Barabara  za Vijijini  na  Mjini  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu  Mhandisi  David  Msechu  amewaomba  Madiwani  Kushirikiana  na  kamati za  maendeleo  za  kata  ili  kulinda  Miundo  mbinu  ya  Barabara  zinazojengwa  ili zidumu  zaidi..

Hayo  ameyasema  katika  kikao  cha  Baraza  la  Madiwani baada  ya  kutakiwa  kutoa   ufafanuzi  wa  Mkakati  wa  TARURA    katika  kuboresha  Miundombinu  ya  Barabara  katika kuelekea  msimu  wa  masika  ambapo  barabara  nyingi  za  Vijijini  zimekuwa  hazipitiki.

Meneja TARURA Maswa- David Msechu
Meneja TARURA Maswa- David Msechu

        

Mhandisi  Msechu  amesema  kuwa  Madiwani  washirikiane  na  Wenyeviti  wa  vitongoji   katika  kuwahamasisha  wananchi  katika  kufungua  Barabara  ambazo  hazifungulia maeneo  ya  vijijini na  Mjini  ili ziingizwe  kwenye  mpango  wa  Bajeti  wa  TARURA  na Kuboreshwa  zaidi   huku  akimpongeza  mwenyekiti wa  Kitongoji  cha  Nyambiti kwa  kuhamasisha  wananchi   wake.

Meneja TARURA Maswa- David Msechu

    

Kwa  Upande  wa  Madiwa  Wameishauri   Wakala   wa  Barabara  za  Mjini  na  Vijijini  TARURA  wilaya  ya  Maswa  kutoa  kipaumbele  kwa  Barabara muhimu za  kiuchumi  ili  ziweze  kupika  kwa  Urahisi  katika  Kusafirisha  Mazao.

Baadhi ya Madiwani -Maswa.

      

Naye  mwenyekiti  wa  Chama  cha  Mpainduzi  wiaya  ya  Maswa  Mhandisi  Paul  Jidayi  amesema  kuwa  kata  yoyote  ikiwa  na  Migogoro  na  changamoto  katika  kuleta  Maendeleo  kwa  wananchi  aliyefeli  hapo  ni  Diwani  na  hana  cha  kujitetea  katika  Chama.

Sauti ya mwenyekiti wa ccm (W) Maswa Paul Jidayi.

               

Aidha  Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Maswa  Mh  Paul  Maige  ameishukuru  Serikali  ya  Awamu  ya  Sita  chini  ya  Rais  Mama   Samia  Suluhu  Hasani kwa  kuwaongezea  Fedha  zaidi  ya  Bilioni  tatu   zitakazoenda  kuondoa  changamoto ya miundombinu  ya  Barabara  na  ujenzi  wa  Mitaro.

Sauti ya Mwenyekiti wa Halmashauri (W) Maswa Paul Maige
Baadhi Madiwani
Mkurugenzi wa Halmashuri (w) Maswa Mh Saimon Berege