Sibuka FM

RC Kafulila awahakikishia wakazi wa kijiji cha Malampaka kutatua Kero zao.

16 July 2021, 1:37 pm

Mkuu  wa  Mkoa  wa  Simiyu    Mh   David Kafulila amewahakikishia  wananchi  wa   Malampaka  na   mkoa   wa  Simiyu kutatua  Kero  zote  zinazowakabili   ili kuendana  na  kasi  ya  Rais   wa   awamu  ya  Sita  Mh, Samia   Suluhu   Hasani.

Mh,   Kafulila  amesema  hayo  wakati  akizungumza  na  wananchi  wa  kijiji  cha  Malampaka  kilichopo  wilaya  ya  Maswa   mkoa  wa  Simiyu  katika  Kampeni  yake  ya  kuzunguka  wilaya  zote  za  mkoa  ili  kusikiliza  kero  za  wananchi  na  kuzipatia  Ufumbuzi..

Sauti ya RC Simiyu- Davidi Kafulila..

              

Aidha  Mh  Davidi  Kafulila  amesema  kuwa  katika  kipindi  cha  siku  mia moja  za   utawala  wa  Rais   Samia  Mkoa  wa   Simiyu  Umepokea  Fedha  nyingi  kwa  ajili  ya  utekelezaji  wa   Shughuli  mbalimbali za  maendeleo  katika  Sekta  za  Afya, Elimu,  Maji,  na  Miundombinu.

Sauti ya RC Simiyu- Davidi Kafulila..

                

Naye  mwenyekiti  wa   Chama  cha  Mapinduzi  wilaya  ya  Maswa   Ndugu  Paul  Jidayi    amesema  kuwa   Mkuu wa  Mkoa  amefanya  Jambo  jema  la  kutoka  Ofisini  kwake  na   kwenda  kusikiliza  kero  za  wananchi  hivyo  wananchi  wawe  huru  kueleza  changamoto  zinazowakabiri  ili  ziweze  kufanyiwa  kazi .

Sauti ya Mwenyekiti wa ccm Maswa- Paul Jidayi.

              

Katika  hatua  nyingine  mkuu  wa  mkoa  wa  Simiyu  Mh  David  Kafulila  amemuagiza  Mkurugenzi  mtendaji  wa  Halmashauri  ya  wilaya   ya  Maswa  Dokta  Fredrick  Sagamiko  kufuatilia  changamoto za  Uzembe   wa  watumishi  katika  sekta  ya Afya   wilayani  Maswa..

Sauti ya RC Simiyu- Davidi Kafulila..

             

Picha za matukio mbalimbali ya mkutano wa hadhara katika kijiji cha malampaka-Simiyu