Sibuka FM

Wananchi wilayani Maswa Mkoani Simiyu walalamikia upatikanaji wa huduma za Afya katika Hospitali ya Wilaya .

15 July 2021, 12:35 pm

Mkuu  wa  mkoa  wa  simiyu  Mh  Davidi  Zacharia  Kafulila  amemuagiza  mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mh ,   Aswege  Kaminyoge  Kufuatilia  Changamoto  ya  mama  wajawazito  wanaoenda  kujifungua  katika  Hospitali  ya  wilaya  ya  Maswa  kutozwa  Fedha.

Maagizo  hayo  ameyatoa  wakati  wa  Mkutano  wa  hadhara  wenye   lengo  la  kusikiliza  Kero  za  wananchi   Uliofanyika  katika  Uwanja  wa  madeko  uliopo  mjini  Maswa.

Sauti ya RC Simiyu- Kafulila

                        

Mh,  Kafulila  amesema  kuwa  moja  ya  maeneo yanayokera  ni   Idara  ya  Afya  hasa  hospitali  ya  wilaya  ya  Maswa  ambayo  imekuwa  ikilalamikiwa  na  wananchi  kwa  utoaji  wa  huduma  duni  ikizingatiwa   hospitali  hiyo  inategemewa  na   wakazi  wengi   wa   mji wa  Maswa.

Sauti ya RC Simiyu – Kafulila

                         

Akipokea  maagizo  hayo  mkuu wa  wilaya  ya  Maswa   Mh   Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa  tayari  baadhi  ya  changamoto  za upatikanaji  wa  Dawa ameshazifanyia  kazi  kwa  kutoa  maelekezo  ya  kupewa   Orodha  ya  dawa  zinazopatika kila  siku..

Sauti ya DC Maswa – Kaminyoge

                   

Akitoa  ufafanuzi  kuhusu  kulipishwa  Fedha  mama  wajawazito, Mganga  mkuu wa  wilaya  Dokta  Mpolo   Adorati   amesema  kuwa huduma  za  mama  na  mtoto  zinatolewa  Bure  lakini   kuna  baadhi  ya  vipimo  ambavyo  mgojwa  anapaswa  kulipia..

Sauti ya DMO Maswa- Dr Mpolo

             

Wakitoa  malalamiko  mbele  ya  mkuu  wa  Mkoa    baadhi ya  wakazi  wa  Maswa  wamesema  kuwa  kuwekuwepo  na  changamoto  katika huduma  za  Afya  katika  hospitali  hiyo  ikiwemo  mama  wajawazito  kutozwa  Fedha  wakati  wa  kujifungua .

Sauti za Baadhi ya wananchi Maswa

              

Hapa chini ni picha mbalimbali za mkutano huo wa hadhara.