Sibuka FM

Simiyu yazindua Mkakati wa kuongeza Tija katika zao la Pamba.

July 6, 2021, 11:57 am

Mkoa  wa  Simiyu  Umezindua  Kampeni  ya  kuongeza  Tija  katika   zao  la  Pamba  ili   kuwainua  wakulima  Kiuchumi.

Kampeni  hiyo   imezinduliwa  na  Waziri  wa  Kilimo    Profesa    Adolf  Mkenda  na  kusema  kuwa  Serikali  haiwezi  kuamua   Bei  ya  Pamba  katika  Soko  la  Dunia  na  Badala  yake  inauwezo  wa  kuamua  mkulima  avune  kilo  ngapi za  Pamba  kama  atalima  kwa  Tija.

Picha ya Waziri Adolf Mkenda
Sauti ya Waziri wa Kilimo Adolf Mkenda

        

Profesa  Mkenda    amesema  kuwa  ili  wakulima  wazalishe  kwa   tija  ni  lazima   kuboresha  Upatikanaji  wa  Mbegu,   bora  wa  mbegu  na  huduma  za  Ugani  na  tayari  serikali  imetenga  Bajeti    kwa  ajili  ya  kuwawezesha  maafisa  Ugani  katika  utekelezaji  wa  Majukumu  yao..

Sauti ya Waziri wa Kilimo Adolf Mkenda

         

Akitoa  taarifa   kwa   Waziri  wa  Kilimo   Mkuu  wa  Wilaya  ya  Busega   Gabriel  Zacharia   kwa  Niaba  ya   Mkuu  wa  Mkoa   wa  Simiyu   Mh,   David   Kafulila   amesema  kuwa  licha  ya mkoa  Kuongoza  kwa  Uzalishaji    wa  zao  la  Pamba  hapa   nchini    bado  tija  katika   zao  hilo  ni  ndogo  sana  ukilinganisha  na  mataifa  mengine yanayolima  zao  hilo.

Picha : DC Busega Gabriel Zacharia
Sauti ya DC Busega Gabriel Zacharia

                 

Mkurugenzi  mkuu  Bodi  ya  Pamba   Nchini  Ndugu   Marco  Mtunga   amesema   kuwa  chanzo  cha  Umasikii  kwa  wakulima  walio  wengi    ni   kilimo  cha  mazoea   chenye   tija  duni  ambacho  kinaenda  kuisha  kupitia   kampeni  hii..

Picha ; Marco Mtunga
Sauti ya Mkurugenzi mkuu Bodi ya Pamba Marco Mtunga

            

Naye   Balozi  wa  Pamba katika  msimu  huu   ambae  pia  ni  Mkuu  wa  Mkoa   Msaafu   Mh   Agrey  Mwanri    amesema  kuwa  sasa  ni wakati   wa   kuachana  na  kilimo  cha  zamani  cha  kumwaga  mbegu  tukutane  kwenye  Palizi   ambacho  hakikuwa na  Tija   kwa   wakulima .   

 

Sauti ya Balozi wa Pamba Agrey Mwanri

Picha za Matukio ya Uzinduzi wa Kampeni ya Kuongeza Tija katika Zao la Pamba mkoani Simiyu