Sibuka FM

Wilaya ya Maswa yaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kipekee.

23 June 2021, 9:55 am

Jamii  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu   imeaswa  kushirikiana  na  vyombo  vya  kisheria  katika  kuhakikisha   inatokomeza  ukatili  kwa  watoto.

Kauli  hiyo  imetolewa  na   Afisa  tarafa, tarafa  ya  Nughu  Ndugu Venance  Saria  kwa   niaba   ya  mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mh,  Aswege  Kaminyoge  wakati  wa   Maadhimisho  ya   siku  ya   Mtoto  wa  Afrika  yaliyofanyika  katika  Uwanja  wa  CCM- Nguzo  Nane Maswa.

Afisa Tarafa- Venance Saria

               

Ndugu  Saria  amesema  kuwa  hali  ya  Ukatili  kwa  watoto   kwa  wilaya  ya  Maswa  siyo  nzuri  kulingana  na   Takwimu  zilizopo  ambapo  amesema  kuwa  mara  nyingi vitendo  vya  ukatili  vimekuwa   vikifanywa  na   watu  wa  karibu.

Afisa Tarafa -Venance Saria

                 

Aidha   Robert   Urasa   akimwakilisha   Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri  wa  Wilaya  ya  Maswa   amesema  kuwa katika  kutekeza  ajenda  ya  2040  lazima  kila  mwananchi  ashiriki  kwa  kutoa   Haki  kwa  watoto  ikiwa  nipamoja  na   kuwatimizia   Mahitaji  yako  ya  Msingi..

Sauti ya Robert Urasa

                    

Awali  akitoa  utanguzi  juu  ya  Maadhimisho  ya  siku  ya  Mtoto  wa  Afrika   Afisa   Maendeleo  ya  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Maswa  Ndugu   Rodgers  Lyimo amesema  kuwa  mara  nyingi  jamii  imekuwa  ikiwachukulia  watoto  kama  watu  wazima  kutokana  na  mwonekano  wa  maumbo  yao.

Afisa Maendeleo- Rodgers Lyimo

              

Kwa  Upande  wa  Wadau  mbalimbali  wamesisitiza   watoto  kupewa   haki   zao  zote  ili  kuondoa unyanyasaji na  Ukatili kwani limekuwa tatito kwa jamii.

Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa Mwaka huu ni TEKELEZA AGENDA 2040 KWA AFRIKA INAYOLINDA HAKI ZA WATOTO.

-Hapa chini ni picha mbali mbali za matukio ya siku ya Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika