Sibuka FM

Jumla ya Vijiji 45 vya Wilaya ya Maswa kunufaika na TASAF awamu ya Tatu kipindi cha Pili.

May 28, 2021, 11:30 am

Jumla  ya  vijiji  Arobaini  na  tano  vilivyopo  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu  vinatarajiwa  kunufaika   na  Mfuko wa  maendeleo  ya  Jamii i – TASAF  kwa  awamu  ya  tatu  kipindi  cha  Pili.

Hayo  yameelezwa  na  Mratibu  wa  TASAF  wilaya  ya  Maswa   Bi, Grace  Tungaraza  wakati  wa  kikao  kazi  cha  Kuwajengea   uelewa   juu  ya  Utambuzi  na  Uandikishaji  wa  kaya   masikini  katika  vijiji  vilivyokuwa  havipo  katika   Mpango  huo.

Sauti ya Grace Tungaraza.

                

Deocles  Leopord  ni  Mwakilishi  wa  mkurugenzi   mtendaji    wa TASAF   makao  makuu  amesema  kuwa  katika  kipindi  cha  kwanza   awamu  ya  tatu    maeneo  mengi  hayakufikiwa  hivyo  katika  kipindi  hiki  cha  pili  kila  kijiji  kitafikiwa  na  walengwa  kutambuliwa.

Sauti ya Diocles Leopord

                 

Aidha  ndugu  Leopord  amefafanua  zaidi   kuhusu  walengwa  na  wanufaika  wa  mpango  huu  wa  kunusuru  kaya  masikini – TASAF  na  Kumshukuru  Mkurugenzi  mtendaji  wa  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Maswa  kwa  kukubali  kutoa   wataalamu  ambao  wataenda  kutekeleza  zoezi  hilo  la  kubaini  kaya  masikini.

Sauti ya Diocles Leopord

Kwa  upande  wake  Mkuu  wa  wilaya  ya  Maswa  ambae  alikuwa   mgeni  rasmi  katika  Mafunzo  hayo  ya   utekelezaji  Mh,  Aswege   Kaminyoge  amesema  kuwa     elimu  itolewe  ya  kutosha  namna  ambavyo  walengwa  watapatikana  ili  kuondoa  malalamiko  yanayojitokeza    kwa   wananchi na  kuongeza  kuwa  awamu  hii  imezingatia  changamoto  zilizojitokeza  katika  awamu  zilizopita.

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge

          

Naye  mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Maswa  Mh, Paul  Maige kwa  niaba  ya  Madiwani   wenzake ameishukuru  serikali  kwa  kuja  na  mpango  wa  kunusuru  kaya  masikini –TASAF   na  kusema  kuwa  zile  changamoto  za  walengwa  kutoonekana  kwenye  Orodha  zitaisha.

Sauti ya Mw/kiti wa Halmashuri Maswa- Paul Maige

      

Picha mbalimbali za Matukio ya kikao kazi cha TASAF – Maswa Awamu ya Tatu Kipindi cha Pili