Sibuka FM

chama cha mapinduzi (ccm) mkoa wa simiyu chapata mwenyekiti mpya

23 May 2021, 8:07 am

Kwenye picha ni mshindi wa nafasi ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Simiyu Bi.Shamsha Mohamed

Chama Cha Mapinduzi (CCM)  mkoa wa Simiyu leo kimefanya uchaguzi  wa kumpata mwenyekiti wa chama hicho ili kuziba nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho  Enock Yakobo aliyefariki februari 23 ,2021.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi huo Wilbroad  Mutabuzi amesema kura zilizopigwa ni 704 na hakuna kura iliyoharibika ambapo amemtaja  Shemsha Mohamed kuibuka kidedea kwa  kura 441 akifatiwa na  Alphonce Kinamhala kwa kura 174 huku  Sakina Omari akishika nafasi ya tatu kwa kura 89.

Sauti ya msimamizi wa uchaguzi Wilbroad Mutabuzi akimtangaza mshindi wa uchaguzi huo

Akitoa neno la shukrani mwenyekiti huyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na kila mmoja huku akiongeza kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kuisimamia ilani ya chama hicho.

Sauti ya Shamsha Mohamed akitoa neno la shukrani kwa wanachama baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi huo

Awali akiongea kwa niaba ya wabunge wa mkoa huo ,mbunge wa Itilima Njalu Silanga amewaomba wanasimiyu hususan kuhakikisha mkoa unazidi kusonga mbele kimaendeleo huku akiongeza kuwa wao ( wabunge) wapo mstari wa mbele katika kiwatumikia wananchi.

Sauti ya mbunge wa jimbo la Itilima Mhe.Njalu Silanga akiongea kwa niaba ya wabunge wa mkoa wa Simiyu

Nae katibu mwenezi wa chama hicho mkoa wa Simiyu Mayunga George amewapongeza wajumbe kwa kufanya uchaguzi kwa utulivu na kufuata  taratibu za chama hicho hatua iliyopelekea kumaliza kwa amani.

“Niwapongeze sana wanachama wote ambao mumeshiriki kikamilifu katika zoezi zima la kumpata mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa mmeonesha ukomavu wa kisiasa kwa kufanya uchaguzi kwa amani hadi tumemaliza na huo ndio msingi wa chama cha mapinduzi asanteni sana “amesema Mayunga George