Sibuka FM

DC Maswa awaasa madiwani kusimamia miradi ya Maendeleo inayotolewa na Serikali.

May 13, 2021, 10:25 am

Mkuu  wa  wilaya  ya  Maswa  Mkoani  Simiyu  Aswege  Kaminyoge  amewataka  Madiwani  kusimamia  Miradi  na  kufuatilia   maendeleo  inayotolewa  na  Serikali  katika  maeneo  yao..

Kauli  hiyo  ameitoa  wakati  akitoa  Salamu  za  Serikali  katika  kikao  cha  Baraza  la  Madiwani  lililofanyika  katika  ukumbi  wa  Halmashauri hapa  Maswa.

Mh  Kaminyoge  amesema  kuwa  Diwani  anapaswa  kujua  Fedha  zote  zinazoletwa  kwenye  kata  yake na  kufuatilia  matumizi  ya  Fedha  hizo..

Dc Maswa Aswege Kaminyoge
DC Maswa

Diwani  wa  viti  maalumu  kupitia  Chama  cha  Mapinduzi   Mh  Pili  Lameck  amesema  kuwa   Madiwa  wanauhusiano  mzuri  na  Watendaji  wa   vijiji ,  kata  na   Halmashauri  hivyo  kuahidi  kuendelea  kutoa  Ushirikiano.

Sauti ya Diwani viti maalum ccm -Pili Lameck

               

Aidha  Diwani  wa  kata ya  Binza   Ndugu   Aroni  Mboje   ameiomba  Serikali  kutatua  changamoto  ya  Mrundikano  wa  wagonjwa  katika  hospitali  ya  wilaya  ya  Maswa   na  kuhoji  utaratibu  wa  waalimu  kuhangaika  na  Madokezo   badala ya  kufanya  kazi  yao  ya  Kufundisha  watoto..

Diwani wa kata ya Binnza -Aron Mboje

             

Akijibu  hoja  hiyo  Mkurugenzi  wa  Halmashauri  ya  Maswa  Dr  Fredrick  Sagamiko  amesema  kuwa   wakuu  wa  Idara  na  wakuu  wa  Shule wataendelea  kushirikiana  na  Kitengo  cha  Manunuzi  cha  halmashauri.

DED Maswa- Fredrick Sagamiko