Sibuka FM

ZAIDI YA WATOTO LAKI NNE KUPATIWA KINGATIBA SIMIYU

10 May 2021, 5:42 pm

Zaidi ya watoto 400,000 wenye umri wa kwenda shule watapatiwa kingatiba mkoani Simiyu lengo likiwa kuwakinga na magonjwa ya kichocho na minyoo tumbo.

Kwenye picha ni mkuu wa wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kminyoge aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Simiyu

Hayo yamesemwa na mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka mkoa wa Simiyu Dkt Ntugwa Nyorobi wakati akiwasilisha mada kwenye kikao cha uraghibishi na uhamadishaji kilichofanyika Mei 7,2021 kwenye ukumbi wa kanisa katoliki lililopo mjini Bariadi mkoani Simiyu.

Sauti ya Dkt.Ntugwa Nyorobi

Naye mratibu wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi  kipaumbele kutoka wilaya ya Busega Nkwaya Shukia amesema maambukizi bado yapo juu ambapo amesema kwa kipindi cha Jan desemba 2021 watoto waliokuwa na minyoo ni 4157 na kichocho ni 365.

Sauti ya Nkwaya Shukia

Lucy Kulong’wa ni afisa elimu wilaya ya Maswa amesema ni bora kuanza na kisababishi cha magonjwa hayo kwa kudhibiti vyanzo vya maambukizi huku akiongeza kuwa kutoa dawa kwa watoto pekee haitoshi ni bora uwepo mkakati wa kutoa kingatiba kwa jamii nzima.

Sauti ya Lucy Kulong’wa

Kwa upande wake programe ofisa mpango wa taifa wa kudhibiti  magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka wizara ya afya Isaac Njau amesema Kanda ya ziwa maambukizi ya magonjwa hayo yapo juu ikilinganishwa na kanda zingine.

Sauti ya Isaac Njau

Katika hatua nyingine  kaimu mratibu mpango wa taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Oscar Kaitaba amesema changamoto kubwa ipo maeneo ya vijijini sambamba na yale ambayo watu wanajishughulisha na kilimo cha kwenye majaruba ,uvuvi ambapo amesema ni rahisi sana mtu kupata kichocho endapo maji yatakuwa yanavimelea vya kichocho.

Awali akifungua kikao hicho mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Simiyu ,mkuu wa wilaya ya Maswa Aswege  Kaminyoge amesema magonjwa ya kichocho na minyoo tumbo yanaongeza matumizi ya rasilimali  zilizopo huku akiongeza kuwa fedha zilizotengwa mkoani hapo zitumike kwa mujibu wa matarajio ili kuleta matokeo chanya.