Sibuka FM

RADI YAUA MTU MMOJA NA KUJERUHI MMOJA

March 31, 2021, 3:42 pm

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ,kamishina msaidizi wa polisi,Richard Abwa amesema kuwa tukio hilo limetokea  mnamo majira ya saa 01:00 usiku wa kuamkia tarehe 29.03.2021 huko katika kitongoji cha cha Nyahanga “A” kijiji cha Bulima ,kata ya Nyashimo  wilayani Busega.

RPC Simiyu ACP Richard Abwao

ACP  Abwao, amemtaja  aliyefariki dunia katika tukio hilo kuwa ni Veronica Seleman msukuma mwenye miaka 11 mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Nyashimo wilayani hapo  baada ya kupigwa na radi akiwa amelala ndani kwako chumba kimoja na mama yake mzazi Keflin Nengo  mwenye miaka 44 msukuma mkazi wa kitongoji  cha Nyahanga “A” kata ya Nyashimo ambaye naye ni majeruhi.

Ambapo katika tukio hilo lililotokea wakati mvua ikinyesha mama mzazi huyo amepata maumivu sehemu ya mgongoni na kifuani na amepelekwa kituo cha afya cha Nassa kwa matibabu Zaidi na hali yake inaendelea vizuri .

INSERT YA RPC ABWAO 

Sauti ya RPC Simiyu