Sibuka FM

Maelfu ya wananchi Mkoa Simiyu wamlilia JPM

March 25, 2021, 3:58 pm

Maelfu ya wananchi mkoani Simiyu wamejitokeza kwa wingi katika misa takatifu ya kumuombea aliyekuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati Dkt.John Pombe Magufuli ikiwa na lengo la kumuombea kwa MUNGU apumzike kwa amani milele.

Akiongoza maelfu ya wananchi wa mkoa wa  simiyu katika misa takatifu ya kumuombea aliyekuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya tano hayati Dkt.John Pombe Magufuli yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Bariadi  katibu wa chama cha mapinduzi ccm mkoa wa Simiyu Bi.Haula Kachwamba amesema kuwa ni vyema watanzania tukawa na mshikamano na utulivu wakati huu wa msiba na kumuunga mkono rais wa sasa Mama Samia.

Katibu ccm mkoa akieleza

Festo Kiswaga ni mkuu wa wilaya ya Bariadi amesema kuwa ni vizuri tukamuenzi hayati John Magufuli kwa mazuri aliyoyafanya kipindi cha uhai wake na kumuunga mkoano Mama Samia ambaye kwa sasa ndiye rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Dc Bariadi akielezea
Dc Bariadi- Festo Kiswaga

Kwa upande wake Paroko Nkunya wa Parokia ya mtakatifu John ya Bariadi amesema kuwa kifo ni fumbo kubwa sana wanadamu.

Baba Paroko Nkunya

Nao baadhi ya viongozi wa dini mkoa wa Simiyu walikuwa na haya ya kunena kufuatia kifo hicho.

Baadhi ya Viongozi wa Dini