Sengerema FM

Waziri wa ardhi azindua baraza la Ardhi Sengerema.

22 March 2022, 4:14 pm

Picha:Waziri wa aridhi Nyumba na maendeleo ya makazi Mh.Dkt.Anjelina Mabula

Waziri wa Ardhi nyumba na Maendeleo ya makazi  Mh, Agelina Mabula  amewataka  watumishi  wa mabaraza  ya ardhi na nyumba ya Wilaya  nchini   kutimiza wajibu wao kwa weledi kwa kuzingatia  sheria ,kanuni ,taratibu  na miongozo iliyopo  na itakayotolewa  ili kuboresha utoaji wa huduma na utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kauli hiyo ameitoa  wakati  akizindua baraza la ardhi la wilaya ya Sengerema wilayani humo  ambapo amesema kuwa   mamlaka za nidhamu hazitasita kuwachukuliahatua za kinidhamu watumishi  wanaoidharirisha serikali kwa kuendekeza viutendo vya rushwa. 

Sauti ya waziri Anjelina mabula akiwaonya watumishi wa mabaraza ya aridhi nchini

Katika hatua  nyingine  Waziri huyo amewaonya  wananchi wanaokimbilia   katika   maeneo ya uwezekaji  kununua viwanja kwa lengo la kulipwa fidia na kusema kuwa  hakuna mtu yeyote atakayelipwa fidia .

Sauti ya Anjelina Mabula akiwaonya tegesha

Nao baadhi ya wananchi Wilayani humo  wamemshukru waziri huyo kwa kuzindua baraza la ardhi kwa kuwa  uwepo wa  baraza hilo wilayani Sengerema imewasaidia kuondokana na adha ya  kusafiri umbali mrefu wa kwenda Mkoa jirani wa Geita kufuata huduma za ardhi katika baraza la ardhi la mkoa huo.

Sauti za Wananchi wa Sengerema kuhusu Baraza la aridhi

Uzinduzi huu umehudhuliwa na viongozo mabalimbali wakiwemo viongozi wa chama cha mapinduzi CCm