Sengerema FM

TASAF yatoa onyo kali kwa watakao tumia fedha za wanufaika kinyume na utaratibu.

28 May 2021, 4:09 pm

Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyotolewa na Tasaf Buchosa…..

Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya tatu kipindi cha pili katika Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema imejipanga kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa watakao bainika kutumia  fedha za Tasaf kinyume na utaratibu.

Hayo yameelezwa na      Bwn,Donard Mzilai kutoka TASAF makao makuu Taifa wakati akitoa mafunzo ya kuwajengea uelewa wawezeshaji wa mpango wa Tasaf katika  ukumbi wa jengo la Hosptal ya Halmashauri ya Buchosa.

Bwn,Mzilai amesema Tasaf imebaini kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika kipindi kilicho pita hivyo kusababisha walengwa kushindwa kunufaika na Tasaf

Katika hatua nyingine amesema Tasaf awamu ya tatu kipindi cha pili itaanza kutoa fedha kwa walengwa kwa njia ya kielekitloniki kwa lengo la kuhakikisha  usalama wa fedha kwa wanufaika

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo kutoka kata mbalimbali na ngazi ya Halmashauri hiyo wameipongeza Tasaf kwa mafunzo hayo kwani yatasaidia wao kufanya kazi kwa weledi huku wakipongeza uwepo wa mfumo wa utoaji fedha kwa walengwa  kwa njia  ya kielekitroniki.

Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Sengerema kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Sengerema Dr,Emmanuel Kipole amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kufanya kazi kwa weledi ili kuondoa malalamiko kwa walengwa.

Tasaf inatarajia  kuvifikia vijiji 15 ambavyo vilikuwa vimebaki  katika Halmashauri hiyo ambapo itakuwa imevifikia vijiji vyote 82 vya Halshauri ya Buchosa

Taarifa zaidi na Katemi Lenatus……….

Sauti ya Mwandishi wetu Katemi Renatus akiriport taarifa hii….