Sengerema FM

Kaya masikini elf6 kunufaika na Tasaf nchini.

26 May 2021, 8:41 pm

Kaimu mkurugenzi Tasaf nchini Bwn. Swaleh Mwidadi akitoa mafunzo ya uelewa kwa watendaji na wawezeshaji wa Tasaf Halmashauri ya Sengerema.

Jumla ya kaya masikini elfu sita nchini zinatalajia kunufaika na mradi wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya pili huku walengwa millioni moja laki nne na elfu hamsini watanufaika na mradi huo.
Hayo yamebainishwa na Bwn Swaleh Mwidad mwakilishi wa mkurungezi mkuu wa Tasaf nchini wakati mafunzo maalum ya kujenga uelewa kuhusu mpango tasaf awamu ya pili kwa wataalamu na wawezeshaji wa mradi ambapo amesema kuwa lengo ni kufikia idadi kubwa ya watanzania wenye sifa.

Mwidadi ameongeza kuwa mradi wa Tasaf awamu ya pili utaendeshwa kwa mfumo wa kisasa ili kuepusha makosa na malalamiko ya kupoteza fedha na kutokufikiwa kwa wakati pesa za walengwa .
Zaidi ya tillio mbili zinatarajia kutumika katika mfuko wa kunusuru kaya maskini nchini Tasaf awamu ya pili.

Zaidi sikiriza taarifa ya Mwandishi wetu…….

Sauti ya mwandishi wetu Tumain John akiriport taarifa hii..