Sengerema FM

Mamba apotea katika mazingira ya kutatanisha,Madiwani watoa maagizo.

7 May 2021, 7:02 pm

Mwenyekiti Halmashauri ya Buchosa Mh Idama kibanzi akitoa mamzi ya baraza lake kwa serkali

Baraza la madiwani Halmshauri ya Buchosa wilayani Sengerema mkoani Mwanza limeitaka Serikali kumsaka mamba aliye uawa na wananchi kisha kupotea katika mazigira ya kutatanisha.

Mjadala huo ambao umedumu kwa takiribani dakika 10   katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la ofisi za Halimashauri Buchosa wakati kikao cha baraza la madiwani  kikiendelea baada ya diwani wa viti maalum Mh. Mwamini Gandama kulieleza Baraza hilo kuwa katika kata ya Bupandwa,mamba ambaye ameuawa baada ya kushambuliwa na wananchi   amepotea katika mazigira ya kutatanisha huku akiwa chini ya uangalizi wa viongozi wa eneo hilo.

Mjadala huo unamuibua Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni diwani wa kata ya Nyanzenda Mh. Idama Kibanzi  na kuiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka kumsaka mamba huyo huku akienda mbali zaidi kwa kuitaka Serikali kuhakikisha inawakamata  wote walio husika katika kumpoteza mamba huyo ambao wanadaiwa kushikiliwa na jeshi la polisi na badaye kuachiliwa huru.

Taarifa zaidi sikiriza hapa chini……..

Taarifa ya Mwandishi wetu Katemi Renatus