Sengerema FM

Zaidi ya million 50 zatolewa kwenye vikundi vya wakinamama Sengerema.

15 April 2021, 6:51 pm

Wakina mama wilayani Sengerema wakisubilia kukabidhiwa fedha za mkopo

Jumla ya milioni hamsini na saba57,200,000/= zimetolewa kwa vikundi 40 vya wanawake wajasiliamali wilayani sengerema mkoani.

Akizungumza na Redio Sengerema Mratibu wa mfuko wa wanawake Wilaya Bi.Noela Yamo amevitaja vikundi vilivyopewa mkopo  ni pamoja na imani lelemama kutoka butonga,wanaufunuo kutoka Ibisabageni  kutona na  asilimia nne kama  serikali inavyoelekeza.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo halmashauri ya Sengerema Bw.Abeli Mosha amesema wanawake ndio wanaobeba majukumu ya familia hivyo amewaomba wanawake waliopewa pesa hizo za mkopo kuzitumia  kwa malengo ya kujikwamua kimaisha.

Hata hivyo wanawake waliopata mkopo huo wameishukuru serikali kwa kutambua changamoto wanazozipitia  katika kuendesha familia na kuahidi kuzifanyia kazi ya uzalishaji.

Aidha serikali inahimiza wanawake kufanya kazi ili kujikwamua katika wimbi la umasikini na kuacha kusubili kupewa pesa za kutunza familia na wanaume wao.

Taarifa zaidi msikirize mwana habari wetu Anna Elias