Sengerema FM

Ripoti ya CAG yatua bungeni Ndugai kuzikabidhi kamati za hesabu za serikali.

8 April 2021, 12:50 pm

Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema ataikabidhi ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  kwa kamati mbili za Bunge.

Amezitaja kamati hizo kuwa ni Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (Laac).

Ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma leo Alhamisi Aprili 8, 2021 muda mfupi baada ya Serikali kuwasilisha taarifa za ukaguzi wa hesabu za wizara, taasisi na mashirika yaliyo chini yao.

Waliowasilisha taarifa ni Wizara ya Tamisemi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ujenzi na Ofisi ya Rais Utumishi.