Sengerema FM

Chakula mashuleni chaongeza ufaulu kwa wanafunzi Buchosa.

8 April 2021, 12:11 pm

Afisa elimu Sekondari Halmashauri ya buchosa Mwl. Buruno Sangwa akielezea mafanikio ya idara ya elimu sekondari

Kufuatia muamko wa wazazi kuhamasika kuchangia chakula shuleni hali iliyopelekea kuongezeka kwa ufaulu kwa wananfunzi katika halimashauri Buchosa.

Afsa elimu Sekondari wa halimashauri hiyo Mwl. Buruno sangwa amewapongeza wazazi kwa kuhamasika katika utoaji wa chakula jambo lililopelekea kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wa sekondari katika halmashauri hiyo.

Katika hatua nyingine Mwl. Sangwa amesema wamejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kutoa mitihani ya majaribio kila siku jambo linalofanya walimu kujituma zaidi katika ufundishaji wa masomo yao.

Aidha Mwl. Sangwa amesema ufaulu umeongezeka kutoka aslimia 68 kwa mwaka 2018 hadi asilimia 85.3 kwa mwaka 2020 na kuongeza kuwa jitihadi za wazazi ndiyo zimefanya kuongezeka kwa ufaulu huo.

Zaidi msikilize hapa Mwl. Bruno Sangwa akizungumzia mafanikio hayo……………….