Sengerema FM

Namungo fc wachezea kichapo cha gori 1-0 dhiidi ya Nkana fc

4 April 2021, 8:08 pm

Mchezaji wa Namungo fc akikabiliana na wachezaji wa Nkana fc uwanja wa Mkapa Dar es salaam

TIMU ya Namungo FC imepoteza mechi ya tatu mfululizo katika Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa 1-0 na Nkana FC ya Zambia jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

 
Bao pekee la Nkana FC  limefungwa na mshambuliaji Diamond Chikwewe dakika ya 69 na matokeo hayo yanaifanya timu ya wana Ruangwa wa mkaoni Lindi iendelee kushika mkia kufuatia kufungwa 1-0 na Raja Athletic Jijini Casablanca nchini Morocco na 2-0 na Pyramids ya Misri jijini Dar es Salaam katika mechi zake mbili za awali.

Nkana sasa ni ya tatu baada ya kukusanya pointi tatu za kwanza leo ambapo nayo imefungwa 3-0 na Pyramids nchini Misri na 2-0 na Raja kwao, Zambia katika mechi zake mbili za awali.