Sengerema FM

Wafanyabiashara mjini wazidi kumulilia Jpm

29 March 2021, 7:54 pm

Mmoja wa wafanya biashara soko la mnadani Sengerema akizungumza na mwandishi wetu

Wafanyabiashara wilayani Sengerema Mkoani Mwanza, wamlilia hayati Dkt John Pombe Magufuli huku wakidai kumuenzi kwa kufanya kazi.

Wakizungumza wakiwa katika Soko la mnadani lililopo kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema wafanya biashara hao wamesema kuwa katika kuendelea na maombolezo ya siku 21 ya msiba wa Dkt. Magufuli wameona nivyema kujitokeza kwa wingi ili kuendeleza kauli mbiu yake ya hapa kazi tu ili kuondokana na  dhana ya kuwa  tegemezi katika jamii.

Aidha wafanyabiashara  hao wamendelea kumuomba Rais Samia Suluhu Hasani kuendelea kuwatetea wafanya biashara wadogo  ili kufanya kazi zao kwa uhuru na haki bila kubugudhiwa.

Sikiliza Taarifa ya mwandishi wetu Dauson Mukyanuzi ikifafanua zaidi……….

T