Sengerema FM

Rais Mh.Samia Suluh Hassan aanza na mkurugenzi TPA

28 March 2021, 12:53 pm

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan

Akitoa Ripoti hiyo Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kicheere  amesema CAG imeendelea kubaini dosari ya matumizi za fedha yanayofanywa na taasisi na mashirika ya umma pamoja na vyama vya siasa.

CAG amesema kati ya hati 900 alizozikagua, hati 800 sawa na asilimia 87 zinaridhisha huku hati 81 zikiwa na mashaka na mbaya ni 10.

Kichere ameyasema hayo leo Jumapili, Machi 28, 2021 wakati akikabidhi ripoti aliyoifanya kwa taasisi za Serikali Kuu, mamlaka ya serikali za mitaa, mashirika ya umma, miradi ya maendeleo na vyama vya siasa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ulioishia Juni 30, 2020.

Baada ya kupokea taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serkali  CAG Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Samia suluhu Hassan amemtaka waziri Jaffo kwenda kusimamia mapato na matumizi ya tamisemi.

Huku akimsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa TPA Eng. Deusdedit Kakoko kupisha uchunguzi wa ubadhilifu wa fedha zaidi shilingi bilioni 3