Sengerema FM

PAROKO AWATAKA WATANZANIA KUMUENZI JPM KWA KUJITOLEA MAISHA YAO KWA WENGINE.

27 March 2021, 12:30 pm

Padre Henry Kibyabo wa parokia ya Yesu Kristo Mfalme mjini Sengerema katika misa ya kumuombea pumziko la milele hayati Dkt. Magufuli

Hayo yamesemwa na paroko wa palokia ya Yesu kristo mfalme iliyopo mjini Sengerema Padre Henry Kibyabo katika misa maarumu ya kumuombea aliyekuwa rais ya jamhuri ya muungano wa Tanzania hayati Dkt. John Pombe Magufuli iliyofanya kanisani hapo.

Padre kibyabo amesema hayati dkt. Magufuli alijitolea kwa watanzania wote bila kubagua Dini,Kabila wala Chama na amepigania maendeleo ya taifa lake kwa kipindi hiki kifupi cha miaka 5 kajenga miradi mikubwa ya kihistoria katika Taifa kama vile Daraja la Kigongo-Busisi kuhamishia makao makuu ya Nchi Dodoma jambo ambalo liliachwa na mwasisi wa Taifa hili Mwal. Nyerere.

Dkt. Magufuli alifariki Dunia Tarehe 17.03 mwaka hu una taarifa za kifo chake zilitolewa na aliyekuwa makamu wake Mh. Mama Samia Suluhu Hassani huku akitaja sababu za kifo chake ni kutokana na maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa takribani miaka10

Dkt. Magufuli amezikwa katika makaburi ya nyumbani kwao Chato Mkoani Geita