Ruangwa FM

KINA BABA WAJIBIKENI WANAWAKE WAFUNGUE MAGOLI

25 January 2023, 8:32 am

“Kina Baba wajibikeni ili wakina mama wafungue magoli wanawake Wengi wanatumia uzazi WA mpango Kwa sababu wanaume hawawajibiki na wengine wanakimbia kulea”

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Ruangwa katika Mkutano kijiji cha nambilanje katika Ziara yake ya kata Kwa kata inayoendelea wilayani Ruangwa baada ya kupata taarifa ya maote ya watoto wa awali Kua 22 huku walioripoti Hadi sasa wakiwa ni 19 Kwa kijiji cha nambilanje na Mkaranga.
DC Ngoma

Ngoma Amesema rasilimali ni watu ili kuweza kukuza uchumi wa wilaya ya Ruangwa na Taifa Kwa ujumla lazima watu wazaliane na watoto waende wakapate elimu kwani serikali inatumia nguvu kubwa kuwekeza katika miradi ya elimu ili watoto wasome.

Aidala Chigogo na Awesa wote wakazi WA nambilanje wameshauri wakinababa Kuacha uvivu na kuwajibika katika majukumu ya kulea familia na sio kukimbia ili wao wafungue njia

Hata hivyo maoni ya kina Baba Wengi wamedai Kua wanawake swala la kupanga uzazi limekua la Siri na wao ndio wanabeba maamuzi ya kujipangia uzazi WA mpango bila kuwashirikisha wanaume lakini pia Hali ngumu ya kiuchumu “hela kuipata imekua ngumu’