Ruangwa FM

Maafisa Elimu Ruangwa wajazishwa mikataba ya makubaliano kusimamia utendaji kazi

24 January 2023, 9:57 am

Katika kuhakikisha ufaulu unaongezeka na kufikia asilimia 100% kama ilivyo malengo ya mkoa wa Lindi na Wilaya ya Ruangwa. Maafisa Elimu kata wilaya ya Ruangwa wamejazishwa mikataba ya Utendaji kazi katika kata zao ikiwa na malengo ya kupima utendaji ulioonyeshwa katika malengo makuu 23 katika mikataba hiyo.

Akiongea wakati wa Ujazaji wa mikataba hiyo zoezi lilifabyika Januari 24, 2023 katika ukumbi wa Halamashauri ya wilaya hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa Mwl. GEORGE MBESIGWE amesema malengo ya kujaza mikataba hiyo ni kupima utendaji wa maafisa hao na kuwataka kila mmoja anatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa makubaliano ya mikataba hiyo ikiwa ni apmoja na kuhakikisha shule za msingi na sekondari zote zinatoa huduma ya chakula kwa wanafunzi.