Ruangwa FM

HOFU YA JANGA LA NJAA WAKULIMA WATAHADHARISHWA RUANGWA

11 December 2022, 6:51 pm

Wakulima wabnaohudumiwa na chama kikuu cha Ushirika RUNALI kinachohudumu katika wilaya za Ruangwa,Nachingwea na Liwale mkoani Lindi, wametakiwa kutumia pesa zao za korosho kununua chakula na kuhifadhi kutokna na uwapo wa dalili ya janga la njaa lililosabishwa na ukame kwa baadhi ya maeneo ya mkoa huo kutozalisha mazo ya chakula msimu huu.

Hatua hiyo inakuja kufuatia mnada wa 8 wa chama kikuu RUNALI uliofanyika disemba 11,2022 katika Kijiji cha mbecha wilayani Ruangwa mkoani Lindi, ambapo makampuni 19 yalijitokeza kutangaza bei zao kwa lengo la kununua zao hilo ambapo jumla ya Kilogramu milioni tatu laki nne na themanini na sita elfu mia nane na thelathini, zimeuzwa kwa bei juu ya shilingi 1945 kwa kilo huku ya bei chini ikiwa ni 1850.

Mikidadi mbute ni Makamo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi, akiwa katika mnawa nane wa zao la Korosho uliondeshwa katika Kijiji cha mbecha wilayani Ruangwa akatumia wasaa huo kuwaasa wakulima kuzingatia matumizi mazuri ya fedha wanazopata kutokana na uuzaji wa korosho hasa kununua chakula kutokana na uwapo wa uhaba wa chakula unaonekana.

“Tunakwenda katika kipindi kigumu na kwa mwaka huu kuna uhaba wa chakula niwaombe wakulima wenzangu tujitahidi fedha tunazopata kutokana na kuuza korosho tukanunua chakula kitusaidie wakati pia tukijiandaa kuingia kuanza uzalishaji wa mazao msimu unaokuja” alisema mbute.

Miongoni mwa wakulima waliohudhuria katika mnada huo wakiwamo Christopher Ibrahim, Zainabu Mponda na Nurudini musa, Pamoja na kuridhia bei katika manada huo wamewaomba wanunuzi kuwahisha malipo ya wakulima huku wakisisitiza baadhi ya bidhaa nazo zipungue bei madukani ili waweze kukidhi.

“wanunuzi hao watulipe kwa wakati lakini pia serikali iangalie namna ya kutusaidia kwa wmakani bei ipande na vile vile waone namna ya kuthibiti mfumuko wa bei madukani maana pesa hii tukipata madukana zinaonekana kidogo kupata mahitaji yanayotosheleza kutokana na mfumuko wa beo” alisisitiza zainabu ambae ni mkulima wa kijiji cha mbecha wilayani Ruangwa.