Ruangwa FM

DC Ruangwa atoa siku mbili wafugaji kuondoka maeneo yasiyo rasmi

17 November 2022, 3:56 pm

Mkuu wa wilaya ya ruangwa Hassan Ngoma amewaasa madiwani kusaidiana katika operation inayoendelea ya kuwafukuza wafugaji wanaoshi katika maeneo ambayo siyo rasmi wilayani Ruangwa

“Oparesheni inaendelea mfugaji ambae Hana baraka za kijiji au ODC anatakiwa kuondoka wilaya ina eneo moja la kipelemende ambalo kuna maboma yanayotambulika pengine na hapo waondoke mara moja Sisi tunakula ugali mbazi sio ugali maziwa”amesema DC Ngoma

DC amesema hayo Leo katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya Kwanza ya mwaka 2022/2023 katika ukumbi WA ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi

Awali madiwani pia walihoji uwepo wa wafugaji kinyume na utaratibu wanakosa Amani katika maeneo Yao ”Nguvu za kupigana Sisi hatuna waondoke wananchi walime Kwa Amani hawatuchangii chochote katika maeneo yetu”amesema Hamisi Ten Ten Diwani kata ya Narung’ombe

Ikumbukwe operashin hii ya kuondoa wafugaji walio katika maeneo ambayo siyo rasmi inaendelea katika wilaya zote za mkoa wa Lindi kulingana na agizo la mkuu wa mkoa wa Lindi Bi Zainab Telack.