Ruangwa FM

DIT – Waanzisha kampeni kuhamasisha watoto wa kike mashuleni kusoma sayansi

19 October 2021, 3:39 pm

Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) wamezindua kampeni ya ya kuhamasisha wanafunzi wakike kusoma masomo ya sayansi ili kuendana na kukua kwa teknolojia itakayowapa fursa zaidi katika uchumi wa viwanda.

Kampeni hiyo imezinduliwa leo octoba 17 wilaya Ruangwa mkoani Lindi, ikiwa ni hatua kufuatia kuwapo kwa idadi ndogo ya wanawake katika kada mbali mbali zinazotokana na elimu ya masuala ya kisayansi, ambapo mratibu wa mafunzo hayo ya mradi wa RAFIC kutoka DIT, Dkt. SINTA MANYELE amesema mlengo wao ni kuongeza idadi ya wanasanyansi huku afisa uhusiano AGNES KIMWAGA akieleza juu ya mwendelezo wa kampeni hiyo.