Ruangwa FM

Namungo yaahidi furaha jumamosi

26 November 2020, 8:16 am

Wachezaji wa timu ya Namungo wakiwa mazoezini uwanja wa Kassimu Majaliwa wilayani Ruangwa kujiandaa na mchezo dhidi ya Sudani.

Klabu ya Namungo yenye maskani yake hapa wilayani Ruangwa mkoani Lindi imeahidi kupambana kufa ama kupona kwenye mchezo wake na timu ya Al Rabita ya Sudani siku ya jumamosi novemba 28 katika uwanja wa Chamazi jijini  Dar es salaam.

Namungo itapambana na timu hiyo kutoka Sudani kwenye mchezo wa awali wa kuwania mzunguko wa kwanza kwenye kombe la shirikisho Afrika , ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Afisa wa benchi la habari la klabu hiyo ndugu Saidi Bakari Mpuna ameyasema hayo jana alipoulizwa juu ya maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo huo muhimu.”Watu wengi wanatuchukulia sisi kama timu dhaifu kutokana na uchanganwetu kwenye michuano ya kimataifa,ila niseme tu kwamba tutawashangaza wengi na kikubwa wasubiri furaha.”

Timu ya Namungo inashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake miaka mitano iliyopita.Kila la kheri Namungo fc.