Ruangwa FM

Mkurugenzi ruangwa aagiza walimu kufundisha kwa bidii

16 November 2020, 7:58 pm

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Ruangwa mkoani Lindi, FRANK FABIAN CHONYA, amewataka walimu kuendelea kufundisha kwa bidii na  kwa mujibu wa kalenda ya masomo inavyowataka, ili kutimiza malengo ya ufaulu waliojiwekea katika halmashauri hiyo.

Chonya ameyasema hayo jumatatu 16/11/2020 alipotembelea kwa kushtukiza majira ya mchana wa saa nane   katika shule ya msingi Nanganga wilayani humo na kukuta wanafunzi wakicheza kwa kukosa walimu wanaoingia kufundisha madarasani, huku walimu waliokutwa kituoni hapo ni watatu ilihali shulehiyo inatajwa kuwa na jumla ya walimu 8.

Aidha katika hatua hiyo pia mkurugenzi huyo alipita madarasani na kuhoji wanafunzi kuhusu idadi ya masomo waliosoma kwa muda huo ambapo kwa darasa la tatu walisema wamesoma somo moja, darasa la sita walitaja kusoma somo moja na kwa darasa la kwanza na pili walikuwa wakifundishwa na mwalimu wao alikutwa darasani.

Inatajwa hali ya kusua sua kwa ufundishaji wa walimu katika miezi ya majira ya mwisho wa  mwaka inatokana na wenda kuhitimu kwa wanafunzi wa darasa la saba, hali ambayo pengine walimu wanamini kuwa kazi kubwa wameifanya tayari , jambo ambalo mkurugenzi huyo ametaja kuwa si sahihi kwakua hata madarasa yanayobaki yana hitaji kufundishwa kwa kuzingatia mipango kazi na siku zilizoaanishwa katika mihula ya masomo.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwl.KASSIM KAMBONA, ametaja kuwapo kwa udhuru ya baadhi ya walimu waliokosekana kazini hapoambapo aleeza  wengine wamepatwa na msiba, na wengine kuuguliwa na hivyo wamelazimika kutokuwepo kituoni hapo kutokana na kuomba ruhusa ili wakashiriki kutatua changamoto zinazowakabili binafsi na kifamilia.

Kwa kujibu wa mihula ya masomo ya mwaka 2020 muhula wa pili utaisha tarehe 18/12/2020 ambapo shule zitafungwa na kupata mapumziko huku zikitegemewa kufungliwa tarehe 11/1/2021 ikiwa ni muhula wa kwanza wa mwaka mpya wa masomo.