Ruangwa FM

Wananchi msihujumu mradi-Dc. Ruangwa

19 October 2020, 12:14 pm

Wananchi wanaofika wilayani Ruangwa kwa ajili ya kazi mbalimbali kwenye mradi wa ujenzi wa barabara ya Nanganga Ruangwa wamenywa kutohujumu ujenzi wa mradi huu kwa kuiba mali mbalimbali ili kuiwezesha serikali kumaliza mradi huo kwa wakati.

Kauli hii ameitoa mkuu wa wilaya ya Ruangwa mhe.Hashimu Mgandilwa alipotembelea eneo la kuegesha magari na uwekaji wa vifaa vya ujenzi wa barabara eneo la Nandagala kuona maandalizi ya ujenzi wa kambi hiyo.

Baadhi ya wananchi waliofika kambini hapo walilalamika juu ya kitendo walichpoita ni ubaguzi wakati wa utoaji ajira kwenye kampuni inayojenga mradi huo ambapo mhe. Mgandilwa aliwasihi kuwa na subira wakati maandalizi ya ujenzi yakiimarishwa.

Mkuu wa wilaya ya ruangwa mhe. Hashim Mgandilwa wa pili kushoto, wa kwanza ni mwenyekiti wa kijiji cha Nandagala aliyetupa mgongo ni katibu tawala na mbele yake ni meneja wa Tanroads mkoa wa lindi.