Radio Kwizera

Rais Samia atamani kuwalipa Wazee Pensheni

May 7, 2021, 6:40 pm

Na; Seif Upupu

Rais Samia Suluhu Hassan amewaomba wazee nchini kuipa muda Serikali ya Awamu ya 6 ili kuangalia hali ya nchi na ya kiuchumi kisha aanze kuwapa malipo ya uzeeni

Akilihutubia Taifa kupitia mkutano wake na Wazee wa Dar es Salaam, Rais Samia amesema anatamani kuwapa Wazee wote nchini walau Pensheni ya Sh Elfu 30 kwa mwaka lakini anashindwa kufanya hivyo kwa sasa kutokana na hali ngumu ya kiuchumi

Rais Samia Suluhu Hassan kabla ya kuzungumza na Wazee hii leo

Amesema kwa sasa Serikali inatekeleza miradi mingi mikubwa ya maendeleo lakini hali ya kiuchumi imeyumba kutokana na mlipuko wa janga la Corona nchini

Rais Samia amesema baada ya serikali yake kujiridhisha na hali ya kiuchumi, Serikali itatoa Pensheni kwa wazee wenye sifa na sio wastaafu pekee lakini pia hata wakulima na wafugaji kwa kuwa Wazee wamefanya mengi kwa maslahi ya taifa.

Katika hatua nyingine Rais Samia amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kukabiliana kwa haraka na vitendo vya wizi na uhalifu vilivyoanza kurejea hivi karibuni.