Radio Kwizera

Mil.500 zaidhinishwa kujenga Mradi mkubwa wa Maji Ngara

May 7, 2021, 6:26 pm

Na; Seif Upupu

Wizara ya Maji imeidhinisha Sh Milioni 500 kwa ajili ya kujenga mradi wa Maji wa Ngara mjini wilayani Ngara mkoani Kagera utakaofikisha maji kwenye vijiji vya Mukididili, Buhororo, Kumuyange na Nyamiaga

Mbunge wa jimbo la Ngara Bw Ndaisaba George Ruhoro ametoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Maji Bungeni jijini Dodoma ambapo pia ameishukuru wizara hiyo

Mbunge wa Ngara Bw Ndaisaba George Ruhoro

Amesema fedha hizo zitasaidia kutatua changamoto ya maji kwenye maeneo hayo na kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kutafuta maji kwa muda mrefu na wakati mwingine kutumia gharama kubwa

Sauti ya Mbunge Ndaisaba akichangia Bajeti ya Wizara ya Maji

Katika hatua nyingine Bw Ruhoro ameitaka Wizara hiyo kuwa na usimamizi endelevu wa Rasilimali za Maji hususani maeneo ya vijijini kwa kuwapa mikataba watu binafsi ama kampuni ili kusimamia miradi ya maji badala ya kuwaachia wananchi

Waziri wa Maji Bw Jumaa Aweso