Radio Kwizera

Kigoma kuwawajibisha watumishi wanaotatiza Uhuru wa Habari

May 3, 2021, 7:39 pm

Na; Phillemon Golkanus

Serikali mkoani Kigoma imesema itawachukulia hatua watumishi wa umma na wakuu wa Taasisi za umma watakaokwamisha upatikanaji wa habari na kuwanyima ushirikiano waandishi wa habari kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mkuu wa wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mlindoko kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishina wa Polisi Thobias Andengenye amesema vyombo vya habari ni muhimu katika kuchangia maendeleo ya taifa.

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Bi Mwanamvua Mlindoko

Amesema vyombo vya habari vimesaidia kuibua changamoto za wananchi na hivyo kuongeza uwajibikaji kwa viongozi na watumishi wa umma kwa mustakabali wa Maendeleo ya wananchi.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Uvinza Bi Mwanamvua Mlindoko

Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini, UTPC Bw Deogratias Nsokolo amesema Umoja huo unakusudia kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan ili kueleza changamoto za waandishi wa habari na kuomba kufanywa marekebisho ya sheria kandamizi kwa waandishi wa habari nchini.

Rais wa UTPC, Bw Deo Nsokolo