Radio Kwizera

Mbunge Ngara aombwa kuwatetea Watumishi

May 2, 2021, 6:22 pm

Na; Seif Upupu

Chama cha Walimu, CWT wilayani Ngara mkoani Kagera kimemuomba Mbunge wa Ngara Bw Ndaisaba George Ruhoro kuendelea kupaza sauti ndani nan je ya Bunge kwa ajili ya kuwatetea walimu na watumishi wengine wa kada mbalimbali wilayani humo

Akizungumza na Radio Kwizera, Katibu wa CWT wilayani Ngara Bw Steven Mutabazi amesema Bw Ruhoro amewatetea walimu hususani kutokana na kitendo cha walimu kukatwa fedha zao kila mwezi na Bodi ya walimu jambo alilodai kuwa linawanyonya na kuwaumiza walimu

Picha wa Walimu wakiwa Pamoja

Bw Mutabazi amesema kuwa walimu wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutopandishwa vyeo, upungufu wa walimu na hali duni ya miundombinu ya elimu

Insert; KATIBU CWT NGARA

Sauti ya Katibu wa CWT Bw Steven Mutabazi

Kwa upande wake Mbunge wa Ngara Bw Ndaisaba George Ruhoro amesema kuwa ataendelea kuwatetea watumishi wa kada zote awapo ndani nan je ya Bunge kwa kuwa kufanya hivyo ni jukumu lake kwa maslahi ya wananchi wa Ngara.

Mbunge wa Ngara Mh Ndaisaba George Ruhoro

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi hapo jana, Rais Samia Suluhu Hassan amesema watumishi zaidi ya elfu 90 watapandishwa vyeo na kuahidi kujitahidi kuongeza mishahara mwakani