Radio Kwizera

Dr Mpango asema Huu ni Muungano unaoishi

April 26, 2021, 11:51 am

Na Seif Upupu

Makamu wa Rais Dr Philip Mpango amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Muungano unaoishi ili kutimiza matakwa na malengo ya Watanzania

Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Muungano leo kwenye Ukumbi wa Chimwaga jijini Dodoma, Dr Mpango amesema licha ya mafanikio ya Muungano lakini bado kuna changamoto kadhaa ambazo hata hivyo hazimaanishi kuwa Muungano sio imara

Makamu wa Rais Dr Philip Mpango

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa pamoja zimetatua changamoto 15 kati ya 25 zilizokuwa zinaukabili Muungano na kwamba jitihada zinaendelea ili kuzitatua changamoto zilizobaki

Makamu wa Rais Dr Philip Mpango akifungua Kongamano la Muungano

Dr Mpango amesema sehemu kubwa ya Watanzania wamezaliwa baada ya Muungano na kwamba serikali inaendelea na jitihada za kukuza uelewa kwa vijana kuhusu Muungano

Maadhimisho ya miaka 57 ya Muungano mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu inayosema “Muungano wetu ni Msingi Imara wa Mapinduzi ya Kiuchumi, Tudumishe mshikamano wetu”