Radio Kwizera

‘Kwa Mpalange’ yampeleka Muumini BASATA

April 19, 2021, 6:48 pm

Na; Seif Upupu

April 8, 2021 Mwanamuziki Mkongwe wa nyimbo za Dansi nchini, Prince Mwinjuma Muumini, Mwana Buguza, Roboti, Kocha wa Dunia aliachia Rekodi yake mpya ya miondoko ya Singeli inayokwenda kwa jina la Kwa Mpalange iliyoibua gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

Prince Mwinjuma Muumini (Robbot)

Video ya wimbo huo pamoja na Audio yake zimeonekana kuzua gumzo hali iliyosababisha Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA kumuandikia Barua rasmi na kumtaka Robot Prince Mwinjuma Muumini kufika ofisi za BASATA kutoa maelezo kuhusu wimbo huo

Licha ya kufika BASATA, Muumini pia ametakiwa kuondoa video ya wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube huku Audio ikiachwa kuendelea kusalia

Kutokana na hali hiyo, Radio Kwizera FM imefanya Mahojiano na Prince Mwinjuma Muumini, Kocha wa Dunia anayefahamika sasa kwa jina la Robot akizungumza na Seif Omary Upupu

Mahojiano ya Muumini Mwinjuma na Radio Kwizera