Radio Kwizera

Wakamatwa na Mifuko ya Plastiki Bukoba

April 9, 2021, 12:58 pm

Na; Anord Kailembo

Wafanyabiashara 15 katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wamekamatwa na Idara ya Afya na Mazingira baada ya kukutwa na mifuko ya Plasitiki inayozuiliwa na Serikali.

Afisa Mazingira wa Manispaa ya Bukoba Bw Tambuko Joseph amesema wafanyabiashara hao wamekamatwa kwenye oparasheni ya kutekeleza agizo la serikali baada ya kuisha kwa muda kutumia vifungashio vya plastiki

Mifuko ya Plastiki inayoendelea kupigwa marufuku

Amesema wafanyabiashara hao wamekutwa na mifuko ya plastiki zaidi ya elfu 4 na kwamba msako unaendelea ili kuwabaini wengine wanaokiuka maagizo ya serikali huku akiwataka wananchi kuwafichua wenye mifuko hiyo

Sauti ya Mkuu wa Idara ya Mazingira Bukoba, Bw Tambuko Joseph

Wafanyabiashara waliokutwa na mifuko hiyo wamesema wameendelea kutumia vifungashio hivyo kwa kuwa vifungashio vilivyopendekezwa na serikali vina gharama kubwa hivyo vinawasababishia hasara