Radio Kwizera

Mbunge wa Ngara alia na Mafuta ya kula

April 9, 2021, 5:46 pm

Na; Seif Upupu

Serikali imetakiwa kuendelea kuboresha sekta ya Kilimo hususani kilimo cha Alizeti na Michikichi ili kukabiliana na tatizo la upungufu wa mafuta ya kupikia

Kauli hiyo imetolewa leo na Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw Ndaisaba George Ruhoro wakati akichangia kwenye Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa kipindi cha miaka mitano, Bungeni jijini Dodoma

Picha na Maktaba – Mbunge wa Ngara alipowatembelea Wananchi

Amesema mahitaji ya mafuta ya kupikia nchini ni makubwa ikilinganishwa na uzalishaji unaofanyika hali inayosababisha serikali kutumia gharama kubwa kuagiza mafuta nje ya nchi

Sauti ya Mbunge akizungumza Bungeni leo

Bw Ruhoro amesema changamoto kubwa katika uzalishaji wa mazao ya Alizeti na Michikichi ni upungufu wa mbegu bora za kisasa zinazoweza kutoa mavuno mengi