Radio Kwizera

Mil 419.8 kujenga Miundombinu ya Elimu Ngara

April 8, 2021, 5:35 pm

Na; Seif Upupu

Jumla ya Sh Milioni 419.8 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu kwa shule za Msingi na Sekondari kwenye Jimbo la Ngara mkoani Kagera

Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw Ndaisaba George Ruhoro amesema kuwa fedha hizo ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi zake wakati wa Kampeni za uchaguzi mkuu uliopita

Mbunge wa Ngara Bw Ndaisaba Ruhoro

Amezitaja shule za msingi zilizotengewa fedha hizo kuwa ni Kanyinya, Kumnazi na Rulenge huku shule za Sekondari zikiwa ni Kabanga, Lukole na Rusumo B

Sauti ya Mbunge akizungumzia fedha za Ujenzi huo

Amesema Shule za Sekondari za Lukole na Rusumo B zimetengewa Sh Milioni 40 kila shule kwa ya ujenzi wa vyumba vya Madarasa. Bw Ruhoro amesema fedha hizo zitakazotumwa wakati wowote kuanzia sasa zitasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kwa wanafunzi na walimu hali itakayochochea maendeleo kitaaluma