Radio Kwizera

Wananchi Buhigwe wampongeza Dr Mpango

March 30, 2021, 5:32 pm

Na; Albert Kavano

Wakazi wa Jimbo la Buhigwe mkoani Kigoma wameeleza kupokea kwa furaha uteuzi wa aliyekuwa Mbunge wao Dr Phillip Mpango aliyekuwa Waziri wa Fedha na Mipango, kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wamesema uteuzi huo unawatia moyo wakazi wa Buhigwe na Mkoa wa Kigoma kwa ujumla hasa kwa kuwa mkoa huo uko mpakani huku ukionekana kama kutengwa

Makamu wa Rais Mteule, Dr Phillip Mpango

Wananchi hao wamesema kupitia nafasi aliyoteuliwa Dr Mpango, wakazi wa Jimbo la Buhigwe wanaamini kuwa itachochea maendeleo yao, mkoa na taifa kwa ujumla

Wakazi wa Buhigwe wampongeza aliyekuwa Mbunge wao

Dr Phillip Mpango anatarajiwa kuapishwa kesho majira ya saa tisa alasiri baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwasilisha mapendekezo ya jina hilo kwenye kikao maalum cha Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM na baadaye jina hilo kuwasilishwa Bungeni na kupitishwa kwa kura 363 sawa na asilimia 100 ya kura zote zilizopigwa