Radio Kwizera

Biharamulo wahimizwa kuwajibika

March 25, 2021, 8:36 am

Na; William Mpanju

Serikali Wilayani  Biharamulo  Mkoani Kagera  imewataka  wananchi na watumishi wa umma kuendelea  kufanya kazi kwa bidii ili kumuenzi hayati  Dr John  Pombe Joseph Magufuli  

Mkuu wa wilaya ya Biharamulo, Kanali  Mathias  Kahabi  amesema hayo wakati  akieleza namna wananchi  wa Biharamulo  wanavyotakiwa  kuendelea kumuenzi  kwa kufanya kazi kama ilivyokuwa kauli mbiu ya Dr Magufuli ya “Hapa Kazi Tu”

Ramani ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera

Amesema Watanzania wanamuamini Rais wa sasa Mama Samia Suluhu Hassan kutokana na jinsi anavyowajibika na kwamba kutokana na kufanya kazi kwa karibu na Hayati Dr Magufuli, atafanikiwa kuifikisha Tanzania pale ilipotakiwa kufika

Kanali Mathias Kahabi akielezea miradi aliyoiacha Dr Magufuli Biharamulo

Aidha Kanali Kahabi amewataka  wakazi wa wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kuendeleza mshikamano, upendo na Uzalendo miongoni mwao ili  kudumisha  amani  na utulivu  kama  sehemu  ya kumuenzi Hayati  Dr  John  Magufuli