Radio Kwizera

Ombi la Waumini wa Kanisa Katoliki Chato.

March 24, 2021, 11:44 am

Na; Elias Zephania

Waumini wa Kanisa Katoliki la Bikra Maria, Parokia ya Chato mkoani Geita wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuendeleza yale aliyoyaacha hayati Dr John Magufuli ikiwemo kudumisha Umoja na Mshikamano wa viongozi wa dini nchini.

Wakizungumza na Radio Kwizera kwa nyakati tofauti waumini wa kanisa hilo wamesema hayati Dr Magufuli amechangia pakubwa katika kukuza masuala ya Kiimani kwa Watanzania kwa kutoa michango ya ujenzi wa makanisa na misikiti bila kujali itikadi yoyote.

Waumini wa Kanisa Katoliki wakifuatilia Ibada

Aidha waumini hao wamesema huu ni wakati wa Watanzania kushikamana bila kujali itikadi za kidini, kikabila, kisiasa wala ukanda ikiwa ni njia ya kudumisha amani ya nchi na Mapinduzi ya Kiuchumi.

Taswira ya Waumini wakiendelea na Ibada
Waumuni wa kanisa katoliki Chato