Radio Jamii Kilosa

UWT Kilosa yatoa msaada mashuka ya wagonjwa kituo cha afya Kidodi

30 May 2023, 11:05 pm

Mwenyekiti wa UWT Kilosa akikabidhi mashuka kwa Mganga Mfawidhi kituo cha afya Kidodi. Picha na Asha Madohola

Katika juhudi za kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha huduma za afya nchini , Umoja wa Wanawake Tanzania UWT wilaya ya Kilosa wametembelea kituo cha Afya Kidodi kuwafariji wagonjwa pamoja na kutoa misaada ya kijamii kama vile sabuni na mashuka na kuwatia moyo madaktari kutokana na utoaji wa bora wa huduma kwa wagonjwa.

“Kituo cha afya Kidodi kimekuwa mojawapo ya kituo kinachotegemewa katika wilaya ya Kilosa kutokana na kutoa huduma bora hususan kwa akina mama wajawazito wamekuwa wakihudumiwa vizuri”.

Kwa kutambua umuhimu wa utoaji wa huduma ya afya kwa wagonjwa katika kituo cha afya Kidodi kilichopo jimbo la Mikumi wilayani Kilosa uongozi wa UWT Kilosa wametoa misaada ya vitu mbalimbali zikiwemo mashuka ya wagonjwa.

Akiwa katika ziara ya kikazi tarafa ya Mikumi Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilosa Bi Jamillah Miyonga alisema kwa kutambua uwepo wa kituo cha Kidodi na utuoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wakina mama wajawazito wakishirikiana na kamati ya utekelezaji waliamua kukipa kipaumbele kituo hicho katika misaada waliyoipokea ili iweze kuwasaida wagonjwa.

“Kwa huduma ambazo zinatolewa kituoni hapa mimi pamoja na kamati yangu ya utekelezaji tumejiridhisha ni nzuri na ndio mana tumekuja hapa kutoa msaada wetu tunaomba muupokee ili kuwatia moyo madaktari na wagonjwa wapate faraja” alisema Bi Miyonga.

Sauti ya Mwenyekiti UWT Kilosa Bi Miyonga
Bi Anisia Ignas akipokea msaada wa sabuni

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Kidodi Dokta Frank Lyimo na Anisia Ignas Mbomi wamewashukuru wanawake hao wa UWT kwa kuwapatia msaada huo ambao waliweza kutambua umuhimu na thamani ya uwepo wao katika kituo hicho hususan katika utoaji huduma bora kwa wagonjwa.

Sauti za Mganga Mfawidhi na Bi Anisia

Awali akiwa katika muendelezo wa ziara yake Mwenyekiti huyo wa UWT wilaya ya Kilosa alisema kuwa wakiwa kwenye utekelezaji wa agizo kutoka taifa ni kufanya uhakiki wa miradi ya maendeleo ambapo walifanikiwa kupitia miradi ya UWT na changamoto iliyopo ni malimbikizo wa madeni na kufanikiwa kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa njia ya control number pamoja na kusajili wanachama wapya wa jumuiya na kuwasajili katika mfumo wa Kidigitali.

Sauti ya Mwenyekiti UWT Kilosa Bi Miyonga
Wanachama wapya waliosajiliwa katika ziara ya Mwenyekiti UWT wilaya ya Kilosa

Naye Katibu wa UWT wilaya ya kilosa Bi Joha Dole alisema kuwa imefika wakati sasa wanawake kuungana kwa pamoja kupinga ukatili ambao unaenea kwa kasi hivyo wanatakiwa kupaza sauti watakapofanyiwa ukatili ama kuona ukatili unafanyika.

Sauti ya Katibu UWT Kilosa Bi Joha

Wakizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti UWT kata ya Mikumi Janeth Ngonyani na diwani viti maalumu tarafa ya Mikumi Mhe Nadya Hassan Mohammed waliwashukuru viongozi hao UWT ngazi ya wilaya kwa kuwatembelea katika tarafa yao na kwamba maagizo yaliyotolewa watayafanyia kazi kuanzia ngazi za matawi.

Sauti za Bi Janeth na Mhe Nadya wakizungumza
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kilosa Bi Miyonga akipanda mti katika kituo cha afya Kidodi
Bi Miyonga akikabidhi kadi ya uanachama kwa mmoja wa wanawake