Radio Jamii Kilosa

Mradi wa BOOST Kilosa kujenga shule mpya Mtumbatu

30 May 2023, 10:14 am

Madarasa ya shule ya msingi Machatu yaliyojengwa na mradi wa Boost. Picha na Glady’s Mapeka

Serikali imedhamiria kuondoa adha za sekta ya elimu nchini kwa kuwaletea mradi wa Boost ambao umeanzishwa kwa makusudio ya uboreshaji wa miundombinu kwa madarasa ya awali na msingi, kuimarisha mapito ya wanafunzi wa awali na msingi kwa kuweka mpango wa shule salama na kuimarisha na kuboresha mpango wa mafunzo endelevu kazini kwa walimu wa madarasa ya awali na msingi mashuleni.

Tumekuwa wa kwanza katika kutekeleza mradi huu wa Boost hivyo ni wajibu wetu kuungana kushirikiana ili kuikamilisha tusipofanya hivyo tutawwanyima wengine kutopatiwa fedha za miradi na hapa tukapunguziwa fedha hivyo lazima tuoneshe kwamba tuna dhamira ya dhati na mradi huu”.

Na Asha Madohola

Wananchi wa kata ya Mtumbatu iliyopo wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro wametakiwa kuupokea na kutekeleza mradi wa Boost kwa kushiriki ipasavyo katika utoaji wa nguvu kazi kwenye ujenzi wa shule mpya ya msingi ambao utapunguza kero ya wanafunzi kusomea nje.

Mbunge wa jimbo la Kilosa Prof Palamagamba Kabudi akizungumzia mradi wa Boost

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mbunge wa jimbo la Kilosa Prof Palamagamba Kabudi aliishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijenga sekta ya elimu nchini ambayo ilikua ikikabiliana na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati.

Prof Kabudi alisema kuwa kata ya Mtumbatu imekua ya kwanza kupelekewa mradi wa Boost ambao upo mahusus kwa kuboresha na kuimarisha elimu ya awali na msingi Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuboresha miundombinu ya madarasa na ili kukamilika inahitaji ushiriki wa nguvu kazi za wananchi.

“Katika mkoa wa Morogoro wenye halmashauri tisa tumepewa shule 17 na halmashauri ya Kilosa tumepewa shule nne katika jimbo la Kilosa shule 3 na Mikumi shule moja kwahiyo ndugu zangu wananchi jambo la msingi ni kujitolea na uwezo huo tunao” alisema Prof Kabudi.

Sauti ya Mbunge Prof Palamagamba Kabudi
Afsa Elimu Msingi Kilosa Bi Zakia Fandey

Akizungumza Afsa Elimu Msingi Wilaya ya Kilosa Bi Zakia Fandey alisema wananchi kata hiyo wanapaswa kujivunia kuwa waanzilishi wa utekelezaji wa mradi huo ambao ukikamilika utaondoa adha ya mrundikano wa wanafunzi katika darasa moja na kwa kuwa mradi huo ni shirikishi wanatakiwa kujumuika kwa pamoja ili kuleta matokeo chanya kwa haraka.

Sauti ya Bi Zakia Fandey Afsa Elimu Msingi
Ndg Nelson Kiliba Mratibu wa Boost Kilosa

Kwa upande wa mratibu wa mradi wa Boost wilayani Kilosa Nelson Kiliba alisema mradi huo umedhamiria uboreshaji wa miundombinu, shule salama, kuwaongezea walimu ujuzi na kwa mwaka huu fedha umeanza kutekelezwa na mradi huo kwa awamu ya kwanza umeanzwa kutekelezwa kata ya Mtumbatu kwa ujenzi wa shule mpya yenye vyumba vya madarasa saba.

Sauti ya Mratibu wa Boost Kilosa ndg Kiliba
Mshauri wa Mradi wa Boost Kilosa Eng Maeda

Naye Eng Eliud Maeda mshauri wa mradi wa Boost alisema wamejipanga vizuri kutoa utaalamu kwa ushauri kwenye kamati ya ujenzi wa majengo ambapo wanatarajia kuwa na majengo yakinifu ambayo yatatumika kwa muda mrefu.

Sauti ya Eng Maeda
Mbunge Prof Kabudi akipokea taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa madarasa Machatu shule ya msingi
Mratibu wa Mbunge Ndg Msakila akiongoza kikundi cha ngoma kijiji cha Machatu
Mbunge Prof Kabudi akisalimiana na wafanyabiashara wa Mtumbatu