Radio Jamii Kilosa

Mwenge wa Uhuru wang’arisha miradi saba ya maendeleo wilayani Kilosa

12 May 2023, 10:45 pm

Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa wilaya ya Gairo Mhe Jabir. Picha na Asha Madohola

Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka wilayani Kilosa yamefanyika wilaya ya Gairo ili kuendeleza falsafa ya Mwenge wa Uhuru kama ilivyoasisiwa na Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere ikiwa ni tunu ya kuleta amani katika Taifa na tumaini kulipokua hakuna matumaini na kuleta upendo palipojaa chuki na kuleta heshima kulipojaa chuki pamoja na kuambatana na ujumbe wa mwenge.

“Tuendelee kuhamasisha falsafa ya Mwenge wa Uhuru kwa kuwarithisha vizazi na vizazi ambavyo vinatakiwa vielewe dhana ya falsafa ya Mwenge wa Uhuru na 2023 mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuja ujumbe unaohusiana na mabadiliko ya tabianchi hifadhi ya mazingira na utunzaji wa vyanzo vya maji”.

Na Asha Madohola

Jumla ya miradi saba ya maendeleo wilayani Kilosa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.4 imezinduliwa na Mwenge wa Uhuru na kujiridhisha matumizi sahihi ya fedha zilizotumika katika ujenzi na usimamizi wa mzuri wa fedha za miradi hiyo.

Miradi yote iliyopitiwa kukaguliwa na kufunguliwa na mwenge wa uhuru imepita kwa kishindo kikubwa katika utekelezaji wake wa usimamizi wa fedha zilizotolewa na serikali bilion 1.2 na wananchi shilingi michango milioni 86.6 huku wahisan wakichangia milioni 600.

Hayo yalizungumzwa na Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka wakati akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya ya Gairo kwenye makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Kilosa Mhe Shaka Hamdu Shaka akizungumza

“Mhe Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amemwaga fedha wilayani Kilosa kwa ajili ya kushamirisha maendeleo endelevu katika sekta ya elimu, afya na miundombinu na tupo tayari kuziheshimu fedha zinazoletwa na serikali na kuunga mkono jitihada za kuleta maendeleo kwa wananchi” alisema Mhe Shaka.

Sauti ya Mhe Shaka Hamdu Shaka
Kiongozi wa mbio za Mwenge Ndg Abdalla Shaib Kaim akizungumza

Kwa upande wake Ndg Abdalla Shaib Kaim kiongozi mkimbiza mbio za Mwenge kitaifa wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru wilayani Gairo aliwapongeza viongozi kwa usimamizi wa miradi ya maendeleo ya Kilosa na kuendelea kufanya kazi kwa umoja na mshikamano katika kutimiza majukumu ya kitaifa.

Sauti ya Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Ndg Abdalla Shaib Kaim

Hata hivyo akiwa katika moja ya mradi wa maendeleo wa upanuzi wa mradi wa maji Dumila alisema kuwa amekagua nyaraka zilizotumika wakati wa ujenzi, kukagua jengo na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.

Sauti ya kiongozi wa mwenge Ndg Abdalla Shaib Kaim

Aidha akiwa katika viwanja vya mkesha wa Mwenge wa Uhuru ndg Abdalla Shaib Kaim alisema kuwa Mwenge wa uhuru umebeba kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa’’, hivyo amewataka wananchi kuiunga mkono serikali kwa kupanda miti na kuacha kuharibu mazingira kwa kukata na kuchoma miti hovyo.

Sauti ya kiongozi wa mwenge Ndg Abdalla Shaib Kaim
Mbunge wa jimbo la Kilosa Prof Palamagamba Kabudi

Naye Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof Palamagamba Kabudi alisema kuwa anaishukuru serikali kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo hususan shilingi bilion 1.7 zilizotolewa kwa ajili ya mradi wa maji Dumila.

Sauti Mbunge wa jimbo la Kilosa Prof Kabudi

Akizungumza wakati akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Gairo Mhe Jabir Omary Makame alikiri kupokea Mwenge wa Uhuru 2023 na viongozi sita wa mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo utakimbizwa kwa kuona, kuzindua na kuweka mawe msingi katika miradi ya maendeleo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Gairo Mhe Jabir Omary Makame

Awali akisoma risala ya utii kwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Katibu Tawala ya wilaya ya Kilosa Mhe Yohana Kasitila alisema kuwa wanapoupokea Mwenge wa Uhuru wanakumbuka maneno ya Hayati Mwalimu Nyerere ya kuleta heshima palipojaa dharau na Kilosa wameendelea kuyaenzi maneno hayo kwa kuleta amani, upendo, mshikamano na utulivu bila ya kuleta ubaguzi wa rangi,kidini na kikabila.

Sauti ya Katibu Tawala Kilosa Mhe Kasitila