Radio Jamii Kilosa

Waliotajwa kwenye ripoti ya CAG waachie ngazi

10 April 2023, 1:37 pm

Katibu wa Uvccm Kilosa Nyansio Gregory. Picha na Idd Manjawila

Waliotajwa katika ripoti ya CAG watakiwa kuachia ngazi za madaraka walizonazo kutokana na ubadhirifu walioufanya kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Serikali imepata hasara kubwa kutokana na watumishi wenye nia ovu na kama Rais alishasema wapishe, kama chama cha mapinduzi chenye kilishasema mpishe sasa mnasubiri kuona nini mtupishe”.

Na Asha Madohola

Katibu wa Uvccm Wilaya ya Kilosa Ndugu Nyansio Gregory amewashauri wale wote waliotajwa katika Ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) Kuachia viti vyao kabla ya kushughulikiwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Katibu Nyansio aliyasema hayo wakati alipokua akiongea na vijana wanaopata mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Kampuni ya Alliance In Motto Global Kilosa.

“Viongozi wote waliofanya madudu katika nafasi zao wanajijua sasa wanasubiri nini kuachia madaraka na naamini ripoti hii ikiwafikia wabunge hawatafumbia macho uozo mlioufanya ni wakati wenu kuondoka wenyewe” alisema Katibu Nyansio.

Sauti ya Katibu wa Uvccm Kilosa Nyansio Gregory

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati ya hamasa Uvccm Kilosa Idd Manjawila aliwataka vijana hao kujiunga na chama cha mapinduzi ili kuweza kuleta nguvu ya maendeleo vijana pamoja na kushiriki katika hamasa maalumu ya mwenge unaotarajiwa kukimbizwa wilayani Kilosa mapema mwezi wa tano 2023.

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa Uvccm Kilosa Idd Manjawila